2 Kings 1:16-17

16Akamwambia mfalme, “Hili ndilo asemalo Bwana: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli wa kumuuliza habari, ndiyo maana ukatuma wajumbe kuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa sababu umefanya hili, kamwe hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” 17 aHivyo akafa, sawasawa na lile neno la Bwana ambalo Ilya alikuwa amesema.

Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yoramu
Yoramu ni namna nyingine ya kutaja jina Yehoramu.
akawa mfalme baada yake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda.
Copyright information for SwhKC